Jumanne 4 Machi 2025 - 21:44
Ayatollah Modarresi: Uislamu una vipengele vyote vya ustaarabu na duara lake linapaswa kupanuliwa

Hawza / Ayatollah Sayyid Mohammad Taqi al-Modarresi ametoa wito kwa Wanazuoni wa Iraq kuwajibika kwa ajili ya kueneza Dini na kueneza Mafundisho yake.

Kwa mujibu wa timu ya Tarjama ya Shirika la habari la "Hawza", Ayatollah Sayyid Mohammad Taqi al-Modarresi, mmoja wa Wanazuoni wa Iraq, katika Mkutano wake na kundi la Mazuwwari wa Hazrat Sayyid al-Shuhada' (amani iwe juu yake) waliokuja kutoka Ulaya, aliwalingania (aliwapa wito wa) kuchukua jukumu la uenezaji wa Dini na kueneza Mafundisho yake, na kufanya juhudi katika kulingania juu ya hilo kwa kufuata njia ya Hadhrat Abul-Fadhli Al-Abbas (amani iwe juu yake) na kuegemea kwenye dhamira na irada ya mwamko na harakati zake zilizobarikiwa.

Ameongeza kuwa: Kanuni za Mwenyezi Mungu katika uumbaji zimewekwa na hazibadiliki, na hilo ni pamoja na Kanuni za wakati na muda ambapo zinahukumu na kutawala juu ya kila kitu katika ulimwengu huu, na moja wapo (ya mambo hayo yanayohukumiwa na kanuni za wakati na muda) ni Ustaarabu wa kimaada katika nchi za Magharibi, ambao leo hii unaishi katika uzee wake.

Ayatollah Sayyid Mohammad Taqi al-Modarresi alisisitiza: Uingizwaji (Uingiaji) wa Kistaarabu wa Mfumo wa sasa unaotawala Ulimwengu ni Uislamu. Kwa sababu Uislamu una vipengele vyote vya ustaarabu kamili na wa kina, na hauna mapungufu makubwa ambayo hutishia tamaduni mbalimbali za kiustaarabu na kuzifanya zitoweke.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha